Mbunge wa Singida Mashariki(CHADEMA) Mh. Tundu Lissu
---
Muda
mfupi kabla ya kumalizika kikao Cha Bunge jioni ya leo mjini
Dodoma,Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu alisimama kutaka
muongozo wa Spika kuhusu Suala linaloendelea kwenye Bunge hilo la
kukusanya Saini za wabunge wapatao 70 ili kupiga kura ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu.
Mh.
Lissu alisema kuwa kitendo cha Spika kutoa uamuzi kwa jambo ambalo
halijamfikia mezani kwake ni kama ukiukwaji wa kanuni na sheria za
Bunge na itaonyesha kuwa kuna majibu yanaandaliwa kwa hoja ambayo
hatakuiona bado hajaiona na kwa kufanya hivyo nikukiuka taratibu.
Baada
ya Mh.Lissu kutaka muongozo huo,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda alisema
kuwa hajasema kwamba suala hilo si halali kufanyika ila alichosema
halitawezekana kwa kikao hiki cha Bunge,kwa sababu linamalizika siku ya
Jumatatu (23 April,2012), kwahiyo itakuwa ni vigumu sana kulifanya
jambo hilo ndani ya Kikao cha Bunge hili.
Aidha
akitoa ufafanuzi zaidi Mh. Spika mara baada ya Mbunge wa Jimbo la
Ubungo,Mh. John Mnyika,kusimama na yeye akitaka muongozo juu ya jambo
hilo hilo ambapo alihoji kwamba,kuna tatizo gani kama watu wakiendelea
kusaini (saini ambazo Mh. Mnyika alisema idadi yake imefikia 66 ) na
kuwasilisha hoja siku ya jumatatu kwaajili ya kujadiliwa Bunge lijalo?
Mh.
Anne Makinda alisema kwamba yeye hajasema kwamba jambo hilo halifai,
"Naomba nieleweke na answered zitaletwa,sasa hivi nilicho kisema!
nikwamba suala hilo haliwezekani kwa Bunge hili kwakuwa jumatatu ndio
linafikia kikomo lakini kama mtaleta kwa kikao kijacho hakuna tatizo"
alisema Makinda.
No comments:
Post a Comment