habari kutoka Mashariki mwa
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema mapigano makali kati ya
wanajeshi na waasi yamesababisha ubakaji wa halaiki na mauaji ya
wanajeshi tisa.
Duru zinasema zaidi ya watu 100 wamebakwa katika
eneo la Mweso lililoko Kivu ya Kaskazini. Zaidi ya raia elfu 80
wamaaninika kukimbia mapigano hayo ambapo pia kuna taarifa za wanajeshi
20 wa serikali kuasi.Walioasi wanaaminika kuwa waaminifu kwa jenerali muasi Bosco Ntaganda anayetakikana na mahakama ya Kimataifa ya jinai-ICC. Ntaganda ameshtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita ambapo anatuhumiwa kuwasajili watoto jeshini. habari kwa msaada wa BBC SWAHILI.COM
No comments:
Post a Comment