RPC Dodoma, SACP Zelothe Steven
--
Mtu
mmoja ambaye hakufahamika, alivamia PUB inayojulikana kwa jina la LADY
MAY PUB akiwa na silaha aina ya Gobole na kumpiga risasi ya mguu wa
kulia katikati ya goti na kifundo cha mguu (enka) mkaanga Chips, Bw.
ALLY S/O KUBULA mwenye umri wa miaka 22, Mnyamwezi.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 24/04/2012 majira ya saa 02:30 usiku katika eneo la LADY MAY PUB barabara ya Iringa, Manispaa ya Dodoma ambapo majeruhi huyu amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma katika wodi namba 11.
Aidha mtu huyo alipora mikoba miwili mmoja ukiwa wa Mheshimiwa Mbunge wa Katavi Viti Maalumu CCM, PUDESIANA D/O KIKWEMBE mwenye umri wa miaka 44, uliokuwa na US Dollar 600 pamoja na fedha tasilimu za kitanzania 180,000/= na Kadi za Benki ya NMB, CRDB na NBC.
Vile vile katika mkoba mwingine mali ya SHARON D/O HUSSEN TULI ambaye ni rafiki wa Mbunge huyo, ulikuwa na simu mbili pamoja na Tshs.100,000/=, ambao pia uliporwa.
Juhudi za kumsaka mtuhumiwa huyo zinaendelea na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma bado linatoa rai kwa wananchi kupitia mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuhakikisha tunawabaini wahalifu na kuwachukulia hatua stahiki.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wamiliki wa Bar zote, kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zinazowaelekeza namna ya kufanya biashara za bar na grocery, ikiwemo kufunga kwa wakati, ili kuepusha vitendo vya uhalifu vinavyoweza kuzuilika.

Imetolewa na:
ZELOTHE STEPHEN - SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
ZELOTHE STEPHEN - SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA
No comments:
Post a Comment