James Ole Millya akihutubia
Katibu
Mkuu wa TLP Same, Heriel Msolo(kulia) akirudisha kadi jana Mbele ya
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana BAVICHA, Ngd Jhon Heche(wa pili
kushoto)na Aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA), Godbless
Lema(Kushoto)
Vijana wakigombea ofa ya kadi 10 za Millya
James Ole Millya akisalimiana na mwanachama wa CCM aliahamia CHADEMA Same jana
Aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA), Godbless Lema akiwasili Same
Wananchi wa Same wakigombea foleni ya kupatiwa kadi za CHADEMA jana
--
Habari na Seria Tuma
CHADEMA
wanaziara ya kichama Wilayani Same kwa siku nne,kuanzia jana hadi
jumatatu chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana BAVICHA, Ngd John
Heche.
Wana
mikutano maeneo tofauti ya Wilaya katika kuimarisha chama hicho.Mkutano
wa jana ulifanyikia viwanja vya Kwasakwasa Mjini Same kuanzia saa 9
hadi saa 12 jioni
Viongozi
waliohudhuria ni pamoja na aliekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema, Mwenyekiti Bavicha, John Heche, Mweyekiti CHADEMA Kilimanjaro,
Augustino Matemu na kiongozi wa vijana Babati, Wilson Mattaka.
Wengine
ni James Ole Millya aliekuwa Mwenyekiti UVCCM Arusha, aliekuwa Mjumbe
wa NEC CCM kutoka Arusha, Ndg Ally Bananga na aliekuwa Diwani wa
Sombetion (CCM). WOte hawa walihamia CHADEMA mapema mwezi huu
Katika
mkutano huo kadi nyingi sana zilitolewa na kuasiniwa na John
Heche..tena zikigombewa kununua. Lema litoa ofa ya kadi 10 kwa kina
mama na Millya nae akatoa ofa ya kuwalipia vijana kumi..
Aliekuwa
Katibu Mkuu wa TLP Same, Ndg Heriel Msolo alirudisha kadi ya TLP na
kupewa kadi ya CHADEMA na Mwenyekiti wa BAVICHA, John Heche
Lema
aliwataka watanzania kutokubali kugwanywa na wanasiasa kwa misingi ya
udini na ukabila au ukanda na kueleza kwamba CHADEMA haipiganii
maslahi ya kundi lolote katika hayo. Akasema hata yeye
hapiganiimaslahi yake binafsi bali ya watanzania.
John
Heche aliwataka watanzania kujitokeza kutoa maoni yao kwa tume ya
Katiba na kuelekeza kuwa wakatae au wazifanyie mabadiliko makubwa
nafasi za uDC au uRC na nyinginezo za kuteuliwa na mtu mmoja. Akadai
pia madaraka ya rais ni makubwa na mamabo mengi yameachwa kwa mtu
mmoja. hali inayohitaji marekebisho ili kuwe na uwajibikaji wa pamoja..
No comments:
Post a Comment