Sunday, April 29, 2012

check jinsi al-shabaab walivyo lipua kanisa NAIROBI

Mripuko kwenye kanisa mjini Nairobi, Kenya, umeuwa mtu mmoja na kujeruhi wengine 10.
Polisi wakilinda maduka Nairobi
Polisi wanasema guruneti lilirushwa kwenye kanisa la God's House of Miracle kwenye mtaa wa Ngara, wakati wa ibada ya asubuhi.
Daktari mmoja katika Guru Nanak Hospital mjini Nairobi, ambako ndiko majeruhi walikopelekwa, aliwaelezea waandishi wa habari majeruhi aliowaona:
"Tumepokea majeruhi 7, mwanamke mmoja aliumia vibaya kwenye mguu wa kushoto, ambao umevunjika mahala kadha.
Mwanamme mmoja alikuwa na majaraha kadha kwenye nyama na tunafikiri amevunja mifupa piya; labda tukimfanyia x-ray tutatambua.
Kuna mama mmoja aliyevunja kidogo kisuguru cha mguu wa kushoto, na wengineo wamepata mikwaruzo-kwaruzo na kujikata-kata."
Kumetokea mashambulio kadha ya maguruneti nchini Kenya tangu mwaka jana pale serikali ilipotuma wanajeshi Somalia kupambana na wapiganaji wa Kiislamu, Al-Shabaab.

Saturday, April 28, 2012

Mji wa Manchester kuwaka moto

Hatumwi mtoto dukani. Ni msemo uliowahi kuusikia mara nyingi, lakini siku ya jumatatu utakua sahihi.
uwanja wa City
uwanja wa City
Ni siku ambapo wababe wawili wa Ligi kuu ya Premier ya England watapambana ikiwa ni kwenye uwanja wa Etihad wa Manchester City.
Baina ya timu hizi zimefunga bao 173 katika Ligi msimu huu tukishuhudia mengi yaliyofungwa na Wayne Rooney, Sergio Aguero, Javier Hernandez na Carlos Tevez.
Majina haya yanakupa ufahamu kua kila upande unaweza kufanikiwa kuchota pointi kutoka uwanja wa Etihad na kwa ushindi apo Etihad pia Ligi ya msimu huu.
Ukitazama orodha ya majina utaingiwa na tamaa ya ya pambano la kuvutia kutokana na washambuliaji wenye mikwaju mikali bila kusahau wanaowalisha mipira ya kupasua nyavu.
David Silva
David Silva
Man.City kwa kipindi kirefu imemtegemea David Silva na bado anaweza kushawishi matokeo ya mechi wakati wowote huku United ikimtegemea mno Antonio Valencia aliyekua na ushawishi mkubwa msimu huu kwa kuvunja ngome nyingi za vilabu mbalimbali.
Vijana wa Roberto Mancini walipoteza muelekeo baada ya siku kuu ya Krisimasi kipindi ambapo kiwango cha mcheza kiungo David Silva kilianza kushuka ingawa hivi sasa klabu yake imerejesha uwezo wa kufunga mabao kutokana na hali yake kua bora kwa sasa.
Antonio Valencia
Antonio Valencia
Na huku kurejea kwa mshtuko kwa Paul Scholes mwezi januari kunaweza kuonekana kama changamoto iliyoiwezesha United kupanda kilele cha Ligi kuu, ingawa mchango wa Valencia kutoka upande wa kulia ni mkubwa mno. Valencia.
Kufuatia jeraha la kisiginio la mda mrefu mapema msimu huu Valenzia alizinduka kwa kupachika wavuni bao mbili kati ya 4-1 dhidi ya Wolves tarehe 10 Disemba.
Kwa uchache, hawa ni wawili kati ya orodha ndefu ya wachezaji wa Manchester mbili zinazotambiana kushinda pambano la jumatatu litakaloamua mshindi wa Ligi ya mwaka huu.
Tuangalie uwezekano wa hali inayoweza kujitokeza ikiwa kwa mfano:
City itashinda - basi timu hizi mbili zitakua sawa kwa pointi kukisalia mechi mbili, wingi wa goli za City ukiiweka klabu hio juu ya kilele.
Droo -na hapa United itahitaji pointi nne kutoka mechi zilizobaki, hata ikiwa City itashinda mechi zote zilizobaki.
Hapa ushindi wa United katika mechi itakayofuata dhidi ya Swansea basi itatangazwa United kua mshindi endapo City itashindwa kuifunga Newcastle ugenini.
Endapo United itashinda pambano la jumatatu basi Ligi itahesabu kombe la 20 la United.

Friday, April 27, 2012

Taswira Za Watu Watatu Waliouawa Kinyama Mkoani Arusha

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) akiongea muda mfupi baada ya kuangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa maeneo tofauti. Wapi kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akiwa na maofisa usalama katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru jana
 Maiti wakiwa wamelundikwa kwenye gari la polisi baada ya kugundulika wametupwa maeneo mbalimbali wilayani Arumeru jana.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo (kushoto) akiangalia miili ya watu wanne waliouawa kinyama na kutupwa maeneo tofauti. Wapi kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye akiwa na maofisa usalama katika eneo la kuhifadhia maiti katika Hospital ya Mkoa, Mount Meru jana. Picha na Mdau Richard Mwaikenda

Jambazi lenye Silaha lavamia Pub Dodoma lajeruhi na kumpora Fedha Mbunge wa Katavi Viti Maalumu (CCM)

 RPC Dodoma, SACP Zelothe Steven
-- 
Mtu mmoja ambaye hakufahamika, alivamia PUB inayojulikana kwa jina la LADY MAY PUB akiwa na silaha aina ya Gobole na kumpiga risasi ya mguu wa kulia katikati ya goti na  kifundo cha mguu (enka) mkaanga Chips, Bw. ALLY S/O KUBULA mwenye umri wa miaka 22, Mnyamwezi.
 
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 24/04/2012 majira ya saa 02:30 usiku katika eneo la LADY MAY PUB barabara ya Iringa, Manispaa ya Dodoma ambapo majeruhi huyu amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma katika  wodi namba 11.

Aidha mtu huyo alipora mikoba miwili mmoja ukiwa wa Mheshimiwa  Mbunge wa Katavi Viti Maalumu CCM,  PUDESIANA D/O KIKWEMBE mwenye umri wa miaka 44, uliokuwa na US Dollar 600 pamoja na  fedha tasilimu za kitanzania 180,000/= na  Kadi za Benki ya NMB, CRDB na NBC.
 
Vile vile   katika mkoba mwingine mali ya SHARON D/O HUSSEN TULI ambaye ni rafiki wa Mbunge huyo, ulikuwa na  simu mbili pamoja  na Tshs.100,000/=,  ambao pia uliporwa.
 
Juhudi za kumsaka mtuhumiwa huyo zinaendelea na  Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma bado linatoa rai kwa wananchi kupitia mkakati wa Polisi Jamii na Ulinzi shirikishi kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuhakikisha tunawabaini wahalifu na kuwachukulia hatua stahiki.
 
Hata hivyo Jeshi la Polisi linatoa  wito kwa wamiliki wa Bar zote, kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zinazowaelekeza namna ya  kufanya biashara  za bar na grocery, ikiwemo  kufunga kwa wakati, ili kuepusha vitendo vya uhalifu vinavyoweza kuzuilika.
 
 Imetolewa na:
 ZELOTHE STEPHEN - SACP
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA

Rais Banda amtimua waziri

Kiongozi mpya wa Malawi Joyce Banda amemtimua Waziri wake wa mashauri ya kigeni, Peter Mutharika, nduguye Rais aliyefariki akiwa afisini.
Bw.Peter Mutharika alitazamiwa kama mrithi wa marehemu kakake katika uchaguzi wa mwaka 2014 wakati ikitazamiwa kua Rais aliyetoweka angestaafu.
Mazishi ya Bingu wa Mutharika
Mazishi ya Bingu wa Mutharika
Mabadiliko haya ya baraza la mawaziri linatokea siku chache baada ya mazishi ya aliyekua Rais.
Bibi Banda alikua ni makamu wa Rais kuanzia mwaka 2009 lakini baadaye akakosana na Rais na kujitokeza kua mkosoaji wake mkali.
Bi Joyce Banda alilazimika kujiuzulu kutoka chama cha Democratic Progressive mwaka 2010 alipokaidi amri ya kumkubali Peter Mutharika awe mrithi wa rais.
Kufuatia kifo cha Bw Mutharika tareh Aprili, kulikuepo na tetesi kua washirika wa waziri wa mashauri ya kigeni wangejaribu kuzuia mkondo wa katiba wa kumkabidhi madaraka Bi Banda,ambaye tangu hapo alikua ameisha unda chama chake.

UN yapanga vikwazo dhidi ya Sudan



Salva Kiir na Hun Jintao
China huenda ikaunga mkono azimio hilo
Marekani imeandaa azimio ambalo limelenga kuidhinisha vikwazo dhidi ya serikali za Sudan na Sudan kusini ikiwa hazitasitisha mapigano mara moja na kurejea kwenye mazungumzo ya amani.
Azimio hilo linaunga mkono pendekezo la Umoja wa Afrika mapema wiki hii.
Muungano wa Afrika umezitaka Sudan na Sudan Kusini kutekeleza mkataba wa amani kwa muundo mpya wa AU.
Azimio hilo linazingatia sana onyo llilotolewa na Umoja wa Afrika ambapo nchi hizo zilitakiwa kuondoa vikosi vyao kwenye mipaka inayozozaniwa katika kipindi cha saa 48.
Hii ni njia moja ya kidiplomasia inayotumiwa kuzuia vita kati ya majirani hao.
Serikali ya Sudan, imelaaniwa kwa kutekeleza mashambulizi dhidi ya Sudan kusini ikitumia ndege zake za kijeshi. Tayari Sudan kusini imeondoa wanajeshi wake kutoka eneo la Heglig ambalo walikuwa wameliteka.
Wanadiplomasia wanasema azimio hilo huenda likaungwa mkono na nchi nyingi kwa kuwa jumuiya ya kimataifa inataka sana kuepuka vita kati ya nchi hizo mbili.
China ambayo inauwezo wa kupiga kura ya turufu kuzuia vikwazo hivyo inaonyesha dalili kuunga mkono azimio hilo.
Hata hivyo huenda hilo likabadilika wakati vikwazo hivyo vitakavyo pendekezwa vitaorodheshwa na Marekani.

Thursday, April 26, 2012

Ni Maafa,Ubakaji, na Uasi DRC


Wanajeshi wa DRC wakimpa buriani mwenzao.
habari kutoka Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinasema mapigano makali kati ya wanajeshi na waasi yamesababisha ubakaji wa halaiki na mauaji ya wanajeshi tisa.
Duru zinasema zaidi ya watu 100 wamebakwa katika eneo la Mweso lililoko Kivu ya Kaskazini. Zaidi ya raia elfu 80 wamaaninika kukimbia mapigano hayo ambapo pia kuna taarifa za wanajeshi 20 wa serikali kuasi.
Walioasi wanaaminika kuwa waaminifu kwa jenerali muasi Bosco Ntaganda anayetakikana na mahakama ya Kimataifa ya jinai-ICC. Ntaganda ameshtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita ambapo anatuhumiwa kuwasajili watoto jeshini.  habari kwa msaada wa BBC SWAHILI.COM

Hukumu ya Charles Taylor leo

Majaji katika mahakama maalum kuhusu vita nchini Sierra Leone, leo watatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu miaka 10.

Charles Taylor
Taylor anasema kesi hiyo ni njama ya kisiasa
Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ikiwemo ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone.
    Ikiwa atapatikana na hatia atakuwa rais mstaafu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa.
Kiongozi huyo wa zamani anadaiwa kufadhili waasi wa RUF.
Zaidi ya mashaidi 100 wamefika mbele ya mahakama hiyo lakini Bw Taylor amekanusha kuhusika na uhalifu huo wakivita na anadai kuwa kesi hiyo ni njama ya kummaliza kisiasa.
Hukumu ya majaji hao inasubiriwa kwa hamu sana na raia nchini Sierra Leone ambao jamaa zao waliathirika sana wakati wa vita hivyo.
Inakadiriwa kuwa zaidi wa watu elfu 50 waliuawa na wengine wakiwemo wanawake na watoto walibakwa na kukatwa mikono au miguu na waasi wa RUF ambao upande wa mashtaka unasema walipata usaidizi wa silaha kutoka kwa Bw Taylor.
Wakati wa vita hivyo, mwendesha mashtaka anasema kuwa Taylor alikuwa kiungo muhimu katika biashara haramu ya almasi kutoka Sierra Leone.
Kesi hii iliodumu miaka mitatu na nusu, hata hivyo huenda isi kamilike leo kwani pande zote wanauhuru wa kukata rufaa ikiwa hukumu hiyo haitawaridhisha.

Tuesday, April 24, 2012

Bweni la Wanafunzi Lateketea Kwa Moto Handeni

 
Taswira za Mabweni yaliyoungua moto 
--
Na Joachim Mushi,
WANAFUNZI takriban 50 wa Shule ya Sekondari Kidereko wilayani Handeni hawana sehemu ya kujihifadhi baada ya bweni lao kuteketea kwa moto pamoja na baadhi ya vifaa vyao vya shule.
Bweni hilo liliteketea kwa moto hivi karibuni majira ya asubuhi baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme kwenye bweni hilo muda ambao wanafunzi wote walikuwa wakiendelea na masomo darasani.
Akizungumza na Thehabari.com eneo la tukio Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Khamis Said amesema vitu vyote vya wanafunzi takribani 50 waliokuwa wakiishi katika bweni hilo viliteketea kwa moto, yakiwemo madaftari ya wanafunzi, nguo, magodoro na vitanda vya mbao viliteketea kwa moto.
“Hatukufanikiwa kuokoa kitu maana baada ya kusikika mlipuko na baadhi ya watu kuona moshi ukitoka ndani ya bweni hilo ambalo muda huo lilikuwa limefungwa tulikuta moto umesha tanda ndani na ukiwaka kwa kasi jambo hali ambayo ilikuwa ngumu kuokoa,” alisema Said.
Amesema kwa sasa wanafunzi hao wanasaidiwa na wanafunzi wenzao kimalazi huku wakiishi kwa shida kutokana na msongamano uliopo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto. “Unajua baada ya ajali walibaki na nguo za shule walizokuwa wamevaa siku hiyo pamoja na madaftari ya vipindi vya siku hiyo tu, vifaa vingine vyote viliteketea kwenye ajali hiyo…shule imetoa baadhi ya fedha na kuwanunulia maitaji kadhaa japokuwa hayatoshelezi” alisema Mwalimu Said.
Hata hivyo alisema tayari uongozi wa idara ya elimu wilaya ya Handeni umetembelea eneo la tukio na wanafanya utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi hao. Hii ni mara ya pili kutokea kwa majanga ya moto shuleni hapo kwani mwaka 2000 wanafunzi walichoma ofisi ya Mkuu wa Shule hiyo baada ya kuzuka kwa vurugu kati yao na uongozi wa shule.
Habari hii imeandaliwa na mtandao wa habari: www.thehabari.com

Waandamana nusu uchi kulalamikia polisi

wanawake Uganda
Kundi la wanawake wamevua nguo, nusu uchi kulalamikia kitendo cha polisi wa Uganda anayedaiwa kumdhalilisha kingono mwanasiasa wa upinzani. Kanda ya video imeonyesha polisi akimtomasatomasa matiti Bi Ingrid Turinawe wa chama cha upinzani cha Forum for Democratic Change (FDC) baadaya kumkamata kuzuia maandamano ya wiki jana.
Naibu kamishina wa polisi Andrew Kaweesa ameomba radhi na kuahidi kufanya uchunguzi kutokana na tukio hilo. Tangu uchaguzi mkuu mwaka 2011 ambapo rais Yoweri Museveni alishinda Uganda imeshuhudia maandamano ya upinzani ambapo wafuasi wengi wameishia celi za polisi.
Tukio la wiki jana lilipelekea kuwepo ghadhabu ya umma ambapo pia lalama zilitanda kupinga kukamatwa kwa Bi Turinawe ambaye ni kiongozi wa tawi la wanawale katika chama cha FDC kinachoongozwa na Kizza Besigye.
Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango amesema wanawake hao waliandamana hadi kituo cha polisi wakiwa vifua wazi na kupeperusha mabango yaliokuwa na maandishi,''utahisi vipi ikiwa sehemu zako nyeti zitafinywa''.Wanawake sita walikamatwa baada ya kukataa kufunika vifua vyao, lakini wakaachiwa huru bila masharti yeyote.

Katibu Mkuu wa UN akemea hatua ya Sudan

Soko moja lilinyeshewa kwa mabomu
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bani Ki Moon amelaani vikali mashambulio ya ndege za Sudan Kwenye mpaka wake na Sudan Kusini.
Bw Ban amesema hali hii inachochea zaidi uhasama kati ya nchi hizo mbili.
Katibu mkuu huyo ametaka Sudan isitishe mashambulio mara moja akiongeza kuwa harakati za kijeshi kamwe haziwezi kusuluhisha mzozo wa mipaka kati ya nchi hizo mbili.
Ndege za kijeshi za Sudan zilishambulia mji wa Bentiu ulioko Sudan kusini na kusababisha maafa ya raia wa kawaida na hasara kubwa kwenye mji huo.
Awali, Rais wa Sudan , Omar al-Bashir, alipuuza uwezekano wa kufanya mazungumzo na Sudan Kusini, kufuatia mashambulio yaliyotekelezwa na wanajeshi wake ndani ya Sudan Kusini.
Bashir amesema jirani wake huyo hakuonyesha nia ya amani na kwamba utawala wa Juba unaamini na vita.
Rais Al Bashir amesema haya wakati akizungumza na wanajeshi wake katika eneo la Heglig, ambalo lilitekwa na wanajeshi wa Sudan Kusini kwa siku kumi.
Tayari wanajeshi wa Sudan Kusini wameondoka eneo hilo
Katika maiezi ya karibuni, kumekuwepo na makabiliano kati ya pande mbili kwenye maeneo yanayozalishwa mafuta ambayo huwa katika mpaka unaozozaniwa, hali iliyozua wasi wasi ya kuzuka kwa vita.
Rais wa Marekani Barack Obama amezitaka nchi hiyo kuanza mazungumo na kumaliza tofauti zao kwa amani.

MISS REDD’S ARUSHA CITY CENTRE kujulikana mei 5 NDANI YA HOTELi YA KITALII YA NAURA SPRINGS


Washiriki wa kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012, wakiwa katika picha ya pamoja,tayari kuchuana vikali Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.katika shindano hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni kwa viti maalum ni sh.25,000/= na kwa viti vya kawaida ni sh 15,000/= 

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa darasani kwenye mafunzo ya nadharia yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo.

Washiriki wa Miss Arusha City Center 2012 wakiwa kwenye mafunzo ya vitendo yatolewayo na chuo cha Udereva na Ufundi,Modern Driving School,ambao pia ni moja ya wadhamini wa shindano hilo

Mashindano ya Ulimbwende ngazi ya kitongoji  Kanda ya kaskazini,Miss Arusha City Center 2012,yanatarajiwa kufanyika Mei  5 2012 ndani ya hoteli ya Kitalii,Naura Springs Hotel iliyopo kati kati ya jiji la Arusha.

Akizungumza leo jijini Arusha,Mratibu wa shindano hilo Bi Upendo Simwita kutoka  kampuni ya Tour Visual Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo,amebainisha kuwa mpaka sasa maandalizi yao yanakwenda vizuri na kila kitu kimekwisha kamililka ikiwemo sambamba na kuwapata warembo ambao mpaka sasa wametimia 20.

Bi Upendo Simwita amesema kuwa wameishakamilisha mchakato wa kuwapata Warembo wenye mvuto na wenye vigezo stahiki,anaongeza kuwa warembo hao wenye ari kubwa ya ushindani,kama waandaji watahakikisha muwakilishi wa Miss Tanzania 2012 anatokea kwenye kitongoji hicho.

“Shindano hilo litakalokuwa la tofauti kubwa na miaka ya nyuma litawakutanisha walimbwende wapatao 20,ambao watachuana vikali jukwaani, na hatimaye kumpata Mshindi wa Miss Arusha City Center”,alisema Upendo.Amesema kuwa kiingilia katika shindano hilo kimepangwa kuwa ni kwa viti Maalum sh 25,000/= na kwa viti vya kawaida sh.15,000/=. Fanya booking yako ya tiketi mapema kupitia namba – 0755975454 au 0713681059.

Kwa upande wa Burudani,Upendo  amesema kuwa kutakuwepo na Msanii mahiri wa Muziki wa kizazi kipya aitwaye Sam wa Ukweli,Muziki wa Asili,Live Band ya Watoto wa Simba pamoja na burudani nyingine  mbalimbali zitakazotolewa na walimbwende wenyewe siku hiyo.

Upendo amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni REDD’S  ORIGINAL,NAURA SPRINGS HOTEL,CLAUDS FM / CLAUDS TV AND MAWINGU CLUB – ARUSHA,BG HORIZON, MODERN DRIVING SCHOOL,MAKO ADVENTURE,SEBE & BEKI FOR LIFE, MWANDAGO INVESTMENT,S.G. RESORT,MEJA LINK LTD,GEO SECURITY,GOLDEN ROSE HOTEL,RIVERSIDE SHUTTLE SERVICES,ARUSHA TRAVEL LODGE,LITTLE ROSES, LA BELLA VISTA,WAKIPAMBWA NA JANETH BEAUTY PAURLOR NA BI. HADIJA HASSAN.

Monday, April 23, 2012

Taswira Za Elizabeth Michael ' Lulu' Alipotinga Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Leo,Kesi Kusikilizwa tena Mei 7


Mshatkiwa Elizabeth Michael |(17), ' Lulu'  akielekea kupanda ngazi na kupandishwa Kizimbani Kesi hiyo  ilikuja kwa ajili ya kutajwa  Upelelezi haujakamilika hiyo ni kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Elizabeth Kaganda alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rita Tarimo  hivyo kesi hiyo  itatajwa tena Mei 7 mwaka huu. Mtuhumiwa amerudishwa rumande.
 Akizindikizwa ndani ya chumba cha Mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam leo
Mshtakiwa akipanda ngazi kuelekea Kizimbani ambalo kesi yake ilitajwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam huku akiwa katika ulinzi mkali kutoka kwa askari  Magereza.Picha na Mdau Khadija Kalili
KWA HISANI YA HAKI-NGOWI

Sarkorzy ashindwa kwenye uchaguzi

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha kisoshalisti nchini Ufaransa Francois Hollande, ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi nchini humo.
Kura nyingi zikiwa zimehesabiwa Bw Hollande tayari amepata asilimia 28 ya kura.
Francois Hollande
Kiongozi huyo anasema wafaransa wanaimani naye
 
 Nicolas Sarkozy anafuatia kwa asilimia 27 hii ikiwa ni idadi ndogo zaidi kwa rais yoyote wa taifa hilo ambaye amewahi kugombea tena kiti hicho.
Haijawahi kutokea kuwa rais aliyemadarakani anashindwa kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.
Na matokeo haya yanampa mpinzani wa Rais Sarkorzy, Francois Hollande nafasi nzuri sana katika duru ya pili ya uchaguzi huo utakaofanyika baada ya wiki mbili.
Hata hivyo kilicho washangaza wengi baada ya matokeo hayo kutangazwa ni idadi ya kura chama kinacho egemea upande wa kulia kilipata.
Kwa makadirio tu, mtu mmoja kati ya wapiga kura watano nchini Ufaransa alikipigia kura chama hicho, hii ikiwa idadi kubwa zaidi ya kura chama hicho cha Front Nationale kilicho pata kwenye uchaguzi wowote nchini humo.
Rais Sarkorzy anasema matokeo hayo yanaonyesha hali ya wasi wasi raia wa nchi hiyo wanayo na ni kura ya maoni dhidi ya utawala wake.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa mpinzani wake ajitokeze kwenye mdahalo kati yao kabla duru ya pili ya uchaguzi huo.
Lakini bila shaka kutokana na uchache wa kura alizopata dhidi ya Rais Sarkorzy, kiongozi huyo wa chama cha kisoshalisti, Francoise Hollande atakuwa makini sana asipoteze kura muhimu.
Bw Hollande anasema wafaransa wanaimani na mradi wake kwa nchi hiyo ambao umelenga kurejesha haki, usimamizi bora wa uchumi wa nchi, ukuzaji wa nafasi za kazi, kulinda viwanda na kujiandaa vyema kwa siku za usoni.
  BBC SWAHILI.COM

Wanajeshi 400 wa Sudan Kusini waripotiwa kuuwawa katika mapigano.

Mzozo juu ya Heglig na vinu vyake vya mafuta vyenye utajiri umepelekea wasi wasi wa vita kamili.
Eneo lililoshambuliwa na bomu na majeshi ya anga ya Sudan huko Sudan Kusini.
Picha AP
Eneo lililoshambuliwa na bomu na majeshi ya anga ya Sudan huko Sudan Kusini.
 
Maafisa wa Sudan  wanajeshi  400 wa Sudan Kusini waliuwawa wakati wa mapigano katika mzozo wa mji  wa Heglig, eneo la kuzalisha mafuta linalodaiwa na nchi zote mbili.
Majeshi ya Sudan Kusini yamekamilisha uondokaji wao Heglig jumapili, wakisema idadi ya askari waliouwawa ni ndogo na  kile Sudan wanachodai. Idadi  ya waliojeruhiwa Sudan ni haiwezekani  kuthibitisha.
Mzozo juu ya  Heglig na vinu  vyake  vya mafuta vyenye utajiri umepelekea  wasi wasi wa vita kamili ikiwa ni chini ya mwaka mmoja baada  ya Sudan kusini kujitangazaia uhuru wake kutoka kaskazini.

Sunday, April 22, 2012

Rais Jakaya Kikwete Aomboleza Kifo Cha Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki


 Rais Jakaya Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu 
Adam Mwakanjuki mapema asubuhi leo April 22, 2012 katika kambi ya JWTZ ya Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange na Mh Aboud wakiangalia wakati jeneza lenye mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki ulipokuwa unaingizwa katika ndege mapema asubuhi leo April 22, 2012 katika kambi ya JWTZ ya Kikosi cha Anga kabla ya kupelekwa Zanzibar kwa mazishi.Picha na IKULU
--------
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dk. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha mwanasiasa mkongwe Brigedia Jenerali Mstaafu Adam Mwakanjuki aliyefariki dunia katika Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo jijini Dar-es-Salaam jana tarehe 19 April, 2012.

Marehemu amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi visiwani Zanzibar zikiwemo za Uwaziri katika Wizara mbalimbali na pia kuwahi kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.


"Pokea rambirambi zangu za dhati kwa kuondokewa na mzee wetu, kiongozi shupavu na mwanamapinduzi imara, ni pengo kubwa kwetu kwani Marehemu amekuwa mshauri wetu mkweli na muwazi, upendo na ucheshi wake pia ilikuwa faraja kwetu wakati wa vipindi vigumu na vyepesi" Rais ameeleza,

"Tutaukosa  ushauri wake, upendo wake na mchango wake katika kila hali"
  Rais amesema na kumuomba Rais Dk. Ali Mohamed Shein kufikisha salamu zake za rambirambi kwa familia, wananchi wote na viongozi wenzake ambao marehemu amefanya nao kazi katika idara zote  serikalini, jeshini, na pia katika Baraza la Wawakilishi.

Marehemu Mwakanjuki alianza Siasa kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964 akianzia katika Chama Cha Afro Shiraz (ASP) na baadae Chama cha Mapinduzi. 


"hatuna budi kumshukuru mwenyezi Mungu kwa mchango wa marehemu wakati aw uhai wake nasi twamuombea mapumziko mema ya milele, Amina" Rais amemuombea Dua na kuiomba familia ya marehemu kuwa na subira wakati huu wakuondokewa na mpendwa wao.

HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

 Mbunge wa Kigoma Kaskazin(Chadema)na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC),Zitto Kabwe
 ----
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012

•    Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
•    Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’

Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 yawabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73 kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa. 
 
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge
isipokuwa tu kama;

(a)    “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa Bungeni;”

Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa “hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa kura za siri”.

Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara taifa.

Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo Bunge litakutana kwa  haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge
yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’ hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.

Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya
hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;
 
 
  …………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

Mheshimiwa zitto kabwe akiwatania wabunge wa ccm

 Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA)na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge Ya Mashirika ya Umma Mheshimiwa Zitto Kabwe Akiwatania wabunge wa CCM kufuatia habari za Mawaziri Nane(8) kuwajibika kwa kujiuzulu nafasi zao Bungeni Mjini Dodoma

Sudan yashambulia kusini ni baada ya salvakiri kuondoa majeshi yake katika visima

Sudan Kusini imeishutumu Kaskazini kuwa imeshambulia kwa mabomu kituo muhimu cha mafuta, ambayo inaonesha mzozo baina ya nchi mbili hizo bado haukumalizika.
Uharibu uliotokea kwenye kisima cha mafuta kwenye jimbo la Unity, Sudan Kusini
Juma lilopita, wanajeshi wa Sudan Kusini waliteka visima muhimu vya mafuta vya Sudan kaskazini, huko Heglig, na kuzusha malalamiko ya kimataifa na msukosuko mkubwa.
Na picha za satalaiti ya Marekani zinaonesha kuwa sehemu muhimu ya miundo mbinu kwenye visima hivo iliharibiwa vibaya.
Siku ya Ijumaa Wasudan Kusini waliondoka, au walitimuliwa kwa mujibu wa taarifa za Sudan.
Na huko kusini, miripuko kadha kwa mpigo ilisikika masafa ya maili kadha.
Sudan Kusini ilisema hilo lilikuwa jaribio la kuharibu mtambo wa kusafisha mafuta katika kisima cha mafuta kwenye jimbo la Unity.
Naibu wa mkuu wa idara ya usalama ya jeshi la Sudan Kusini, Jenerali Mac Paul, alisema kulitokea mapambano kidogo baina ya wanajeshi wake na wale wa Kaskazini, karibu na mpaka wenye utatanishi.
Haikuwezekana kupata taarifa ya jeshi la Sudan.
Lakini ni wazi kuwa Sudan Kusini ina wasiwasi kuwa itashambuliwa na Sudan.
Juma hili Rais Omar el Bashir amesema anataka "kuikomboa" Sudan Kusini kutoka "wadudu" wanaoingoza nchi hiyo.
Alikasirika baada ya Sudan Kusini kuviteka na kuvikalia kwa juma zima visima vya mafuta vya Heglig, chanzo cha pato kubwa kwa serikali ya Khartoum.
Makamo wa rais wa Sudan Kusini, Riek Machar, aliiambia BBC kwamba wanajeshi wake wako tayari kuiteka tena Heglig, iwapo watashambuliwa tena.

Check Iran yaunda ndege isiyohitaji rubani

Iran inasema imeanza kuunda ndege ya ujasusi sawa na ile ya aina ya Sentinel ya Marekani, ambayo ilianguka nchini Iran mwaka jana.
Mwanajeshi wa Iran anaonesha ndege ya drone ya marekani
Wakuu wa Iran wanasema wamepata maelezo kuhusu namna ndege hiyo inavofanya kazi, kwa kufumbua fumbo la software yake; na sasa inaelewa kikamilifu muundo wa ndege hiyo.
Kuna wasiwasi kuwa Iran huenda ikaweza kuigiza rangi maalumu ambayo inasaidia kufanya ndege hiyo isionekane na vyombo vya radar.
Ndege hiyo ya aina ya Sentinel isiyohitaji rubani, inatumiwa sana na Marekani kugundua maficho ya makundi ya wapiganaji nchini Afghanistan

Salva Kiir awaondoa wanajeshi Heglig

Wanajeshi wa Sudan Kusini
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir ameamrisha wanajeshi wake kuondoka kwenye visima vya Heglig katika mpaka unaozozaniwa kati yake na Jamuhuri ya Sudan.
Wanajeshi wa Sudan Kusini waliteka eneo la Heglig wiki jana ambapo walilaumu utawala wa Khartoum kutumia mahala hapo kama ngome ya kufanya mashambulio.
Hapo Alhamisi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki moon alitaja kuwepo kwa wanajeshi wa Sudan Kusin kama kinyume na sheria ya kimataifa.
Hata hivyo Umoja wa Mataifa ulitaka Jamuhuri ya Sudan kusimamisha mashambulio dhidi ya Sudan Kusini .
Makabiliano kati ya pande zote yalitishia kuzuka kwa vita vingine. Sudan Kusini ilijiondoa kwa Jamuhuri ya Sudan mwaka jana kufuatia muafaka wa amani ulioafikiwa mwaka 2005 baada ya vita vya zaidi ya miongo miwili.
Hapo Alhamisi, Sudan Kusini ilitoa taarifa na kusema haikuwa na haja ya vita na jirani yake na kusisitiza ingewaondoa wanajeshi wake kutoka Heglig pale Umoja wa Mataifa utatuma waangalizi wake.
Awali rais wa Sudan Omar al-Bashir alitishia kuizima serikali ya Sudan Kusini baada ya kupoteza eneo la Heglig ambalo huzalisha zaidi ya nusu ya mafuta ya Sudan.
Chini ya sheria za kimataifa, Heglig ni sehemu ya Jamuhuri ya Sudan japo mipaka kamili ingali kutambuliwa rasmi.

CHECK..orodha yawabunge wliopiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu

 

Kujiuzulu mawaziri ngoma nzito  Send to a friend

WAKATI kishindo cha shinikizo la kutakiwa kujiuzulu mawaziri nane wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kikizidi kurindima, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Serikali itatoa tamko lake rasmi kesho.

Awali Katibu wa Wabunge wa CCM, Jenister Mhagama aliwaambia waandishi wa habari juzi usiku kuwa chama hicho kimefanya maamuzi magumu ambayo yangetangazwa na Pinda mjini hapa jana.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Pinda alipoombwa na waandishi wa habari jana kuzungumzia sakata hilo, hakukanusha wala kukiri kuwapo kwa azimio hilo zaidi ya kusema wananchi wasubiri hadi kesho atakapotoa taarifa rasmi.
Alipoulizwa kama kuna mawaziri ambao wameshawasilisha barua zao za kujiuzulu hadi kufikia jana mchana, Pinda alijibu kwa kifupi kuwa ‘bado hatujapokea, lakini kama wapo watatuletea tu”.
Ingawa Waziri Mkuu hakukiri kupokea barua yoyote, taarifa zisizo rasmi, zilisema mawaziri watano waliokumbwa na msukosuko huo wamekabidhi barua zao huku Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami akikataa kufanya hivyo.

Mwingine ambaye anatajwa kuwa hajawasilisha barua yake, ni Waziri wa Fedha Mustapha Mkulo ambaye kwa sasa yuko nje ya nchi.
Chami ajitetea

Dk. Cyril Chami amesema hataandika barua ya kujiuzulu wadhifa huo na kusema anawaachia wananchi wapime kama kweli anastahili kujiuzulu ama la.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana alisema yuko tayari kujiuzulu endapo tu wananchi na wabunge  watampa fursa ya kusikiliza utetezi wake na kama bado wataona ana makosa,yuko tayari kuachia ngazi.
Dk Chami ni mmoja wa mawaziri ambao Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kikao cha Wabunge wa chama hicho, kimewapa muda hadi kufikia kesho wawe wameandika barua za kujiuzulu.
Kiini cha D. Chami kutakiwa kujiuzulu, ni kauli za Wabunge wa CCM kuwa anamkingia kifua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Charles Ekelege anayetuhumiwa kwa ufisadi.
Hata hivyo Dk Chami alisema hadi jana wizara yake ilikuwa haijapatiwa ripoti ya Mamati Maalumu ya Bunge ya Mashirika ya umma iliyokwenda kumchunguza Ekelege katika nchi za Hongkong na Singapore.
“Nataka wananchi wanielewe nitamwajibishaje Ekelege wakati ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyomchunguza mimi sina…ningejengaje hoja kwa Rais bila kuwa na tuhuma zake?”alihoji D. Chami.
Alisema Mkurugenzi wa TBS ni mteule wa Rais na kuna taratibu zake ambapo taarifa ya kamati hiyo ndiyo ingeisadia Bodi ya Wakurugenzi ya TBS kumjadili na kupitisha maamuzi,”alisema.
Alifafanua hata ripoti maalumu ya ukaguzi iliyofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) hawakuwa wamepewa na wamepatiwa siku tatu zilizopita mjini Dodoma.
“Bado najiuliza CAG alikuwa na agenda gani na wizara yangu kwa sababu hakutupa ripoti yake lakini akawapa baadhi ya wabunge mpaka tulipofuatulia juzi baada ya kelele za wabunge”alisema.
Aliongeza kusema Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, leo anashutumiwa kwa kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma(CHC) bila kufuata utaratibu.
“Utashangaa leo Mkulo anashutumiwa kwa kutofuata taratibu kumsimamisha Mkurugenzi Mkuu wa CHC lakini leo mimi nashinikizwa nimsimamishe kazi Mkurugenzi wa TBS bila kufuata taratibu,”alisema.
Dk Chami alisema amejitahidi kuomba taarifa hiyo ya Kamati Teule iliyomchunguza Ekelege lakini hadi jana hajapatiwa zaidi ya kuambiwa ilipelekwa kwa Spika na hajaambiwa baada ya hapo ilikwenda wapi.
Hata hivyo habari za uhakika ambazo gazeti hili inazo , zinaonyesha kuwa baada ya ripoti hiyo ya kamati kufika kwa Spika, Spika naye aliipeleka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Katika kuthibitisha Wizara ya Viwanda na Biashara haikuwa imeipata barua hiyo, Februari 2,2012 Katibu Mkuu, Joyce Mapunjo alimwandikia barua Katibu wa Bunge akimkumbusha awapatie ripoti hiyo.
Barua hiyo yenye kumbukumbu namba GA96/352/01 iliyopelekwa kwa Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilila, ilisema”nimeona nikukumbushe unisaidie ripoti hiyo niweze kutekeleza maagizo ya kamati”.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, Februari 10,2012 Kamati za PAC na POAC na ile ya Viwanda na Biashara zilikutana Dodoma ambapo Kamati iliendelea kumtuhumu Mtendaji Mkuu wa TBS.
Katika kikao hicho, wizara iliagizwa kuwasilisha kwa CAG ripoti ya idadi ya magari yaliyokaguliwa na mapato yake, na wizara ikakabidhi ripoti hizo  Februari 15,2012 kwa barua yenye kumb GA.96/352/01.
Ni kwa maelezo hayo, Dk. Chami alidai tangu wakati huo ofisi yake haijawahi kupokea ripoti nyingine yoyote iwe ya CAG au kutoka kwa Spika zaidi ya kufahamu kuwapo kwake bungeni wiki hii.
Dk Chami alifafanua kuwa kukosekana kwa ripoti hizo kulimfanya afungwe mikono ya kwenda kwa Rais kumshauri amuondoe Ekelege kwa kuwa hakuwa na ripoti iliyokuwa ikionyesha tuhuma zake.
Kutokana na msingi huo, Dk. Chami alisema chombo alichobakia nacho kuchukua maamuzi ni Bodi ya Wakurugenzi ya TBS na bodi hiyo iliundwa na kuzinduliwa Machi 29, 2012.
Dk Chami alisema bodi hiyo ilikutana Aprili 5,2012 na Wizara yake ikapokea ushauri wa Bodi hiyo Machi 19,2012 na wakati ripoti ya ukaguzi maalumu wa CAG akiipokea Aprili 18 akiwa Bungeni Dodoma.

 


Omari Nundu
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi,Omari Nundu jana alitumia Bunge kurusha kombora kwa Kamati ya Mindombinu kuwa imekuwa na taarifa zisizo sahihi.
Nundu alisema taarifa zote juu yake ni za uongo huku akikanusha kwamba hajawahi kusaini makubaliano (MoU) yoyote kuhusu mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam gati  namba 13 na 14.

Ngeleja
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye pia ni Mbunge wa Sengerema, alipoulizwa na mwandishi wetu kupitia ujumbe mfupi wa maandishi(SMS) alijibu kwa kifupi ‘Tuziachie mamlaka za maamuzi”.
Mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu ili kuinusuru Serikali ni Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo,Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige.
Wengine ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu.
Taarifa zilizopatikana juzi usiku zilieleza kuwa katika kikao hicho, mawaziri hao kwa pamoja waliwekwa katika eneo maalumu na wakawa wakiitwa mmoja mmoja kwa ajili ya mahojiano na wabunge na baadaye kupewa msimamo wa chama.
Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Waziri Mkuu akaendesha kikao kingine cha faragha, safari hii kikimhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Frederick Werema na Waziri William Lukuvi.

Wengine walioitwa katika kikao hicho ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM, Mwigulu Mchemba,Katibu wa Oganaizesheni na Mahusiano ya Nje Januari Makamba na Katibu wa wabunge wa chama hicho, Jenister Mhagama.

Hata hivyo mwenye mamlaka ya kuwafukuza Mawaziri kwa mujibu wa Katiba ni Rais Jakaya Kikwete aliyewateua ingawa hata hivyo badhi ya wabunge wanamtuhumu Rais kuwa si mtu wa kufanya maamuzi haraka na kwa shinikizo.

Jana baadhi ya mawaziri wanaotakiwa kuachia ngazi waliingia katika ukumbi wa Bunge na kukalia viti vyao lakini mara baada ya kuahirishwa kwa kikao, waliondoka haraka katika viwanja vya Bunge.

Baadhi yao walipotafutwa  kwa simu ili watoe ufafanuzi na msimamo wao kuhusiana na azimio hilo la CCM, ama simu zao zilikuwa hazipatikani kabisa na zingine hazikupokelewa, zilikatwa.

Zitto aendelea kutafuta saini

Katika hatua nyingine,Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alisema hoja ya kumpigia Waziri Mkuu kura ya kutokuwa na imani ipo pale pale kama mawaziri wanaotajwa kwa ufisadi hawatajiuzulu kufikia kesho.
“Sisi tunasema bila kumwajibisha Waziri Mkuu hawa mawaziri waliotajwa hawatatoka na wasipotoka madudu haya yatarudia…kwa hiyo ni wao mawaziri kupima na kuwajibika au wamweke reheni Waziri Mkuu,”alisema.
Mbunge huyo alirejea wito wake wa kuwaomba wabunge wenye uchungu na ubadhirifu na ufisadi waunge mkono utiaji wa saini hizo na kwamba kama mawaziri watajiuzulu ifikapo Jumatatu, wataondoa hoja hiyo.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Kambi rasmi ya upizania Bungeni, Freeman Mbowe alirejea msimamo wake wa kuomba kufanyiwa mabadiliko ya katiba ya nchi na kanuni za Bunge ili Spika asiwe anatokana na chama chochote cha siasa.
Mbowe alitoa kauli hiyo kutokana na kile alichodai,  hatua ya Spika Anne Makinda kutafsiri vibaya kanuni za Bunge na Katiba ya nchi ili tu kuilinda Serikali na Waziri Mkuu wake ili asipigiwe kura ya kutokuwa na imani.
“Mambo ya ajabu sana eti Spika anasema hili zoezi letu ni batili…sisi tunamshangaa, wanasheria wanamshangaa na hata wananchi wanamshangaa… anatoleaje mwongozo kwa kitu ambacho hakipo mezani kwake?”alihoji.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, alisema kanuni inataka ili hoja ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu iweze kufikishwa ofisi ya Spika, ni lazima ipate sahihi za wabunge 70 na ndicho wanachokifanya.

Wasomi wazungumza

Baadhi ya wasomi wa Chuo Kikuu wamelitaka Bunge kufuata sheria na kanuni za Bunge kabla ya kufanya maamuzi hayo kwa sababu mawaziri hao wanaripoti kwa Rais Jakaya Kikwete na si Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, wasomi hao walisema kuwa, kutokana na hali hiyo wabunge hao wanapaswa kufuata kanuni ili waweze kutambua kuwa mwenye mamlaka ya kuwaondoa mawaziri hao ni  Rais na si Waziri Mkuu, hivyo basi kumlazimisha aondoke madarakani ni sawa na kumuonea.

“Mimi naona wanamuonea bure Waziri Mkuu Pinda, kwa sababu hana mamlaka ya kuwaondoa Mawaziri madarakani badala yake wanatakiwa kuangalia kanuni kwanza ndipo waweze kufanya maamuzi,”alisema Profesa Simon Mbilinyi mwasiasa mstaafu nchini.

Aliongeza kutokana  na hali hiyo wabunge hao walipaswa kumuandikia barua Rais Kikwete na kumtaarifu kuwa mawaziri wake wameshindwa kufanya kazi badala yake wanatakiwa kuwajibika kulingana na makosa waliyofanya.

Alisema kutokana na hali hiyo maamuzi ambayo yangeweza kutolewa na rais yangekuwa sahihi kwa sababu yamefuata sheria na taratibu zilizotungwa na Bunge.

Alisema kitendo cha wabunge hao kumshinikiza Waziri Mkuu kujiuzulu au kuwaondoa mawaziri hao ni kinyume na sheria na ni sawa na kumuonea, jambo ambalo linaweza kumfanya afanye maamuzi bila ya kufuata taratibu.

Hata hivyo, Profesa Abdalah Safari alisema kuwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) ni wanafiki, na kwamba wanashindwa kufanya maamuzi mpaka wasubiri nguvu kutoka kwa wapinzani.

Alisema kutokana na hali hiyo wabunge hao wamepoteza mwelekeo na kwamba wamejaa woga jambo ambalo limesababisha kuendekeza ufujaji wa mali za umma kwa makusudi.

Naye Makamu Mkuu Chuo Kikuu cha Matakatifu Agustino cha Mwanza (Sauti) Dk  Charles Kitima amesema  mchakato unaofanywa na wabunge kwa   lengo la kumg’oa Waziri Mkuu Pinda sio suluhu ya kutibu tatizo la uwajibikaji kwa viongozi  serikalini.

 “Tunalia watu wajiuzulu wakati tumebaki na mfumo ambao unaruhusu siasa chafu, Mahakama inaingiliwa katika maamuzi yake Tume ya Uchaguzi haiko huru, hili haliwezi kuleta mabadiliko sababu Rais atateua mtu mwingine kufanya kazi hiyo na shughuli zitaendelea kama kawaida”alisema Dk Kitima.

Dk Kitima ambaye alikuwa akichangia  mada  katika kipindi cha jicho letu katika habari kinachorushwa na kituo cha Televisioni cha Star Tv cha jijini Mwanza jana, alisema njia pekee ambayo inaweza kuleta  mabadiliko ni kubadilisha mfumo utakaowezesha viongozi kuwajibika kwa wananchi.

“Walijiuzulu Edward Lowasa, Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha nini kimebadilika, rais ameteua wengine matatizo bado yanaendelea serikalini tatizo si watu bali mfumo uliopo ambao unatoa fursa kwa viongozi na watendaji kuwajibika kwa waliowateua”alisema Dk Kitima.

Habari hii imeandikwa na Daniel Mjema na Habel Chidawali, Dodoma, Patricia Kimelemeta, Geofrye Nyang’oro

Orodha ya wabunge waliosaini:
      
  1. 2.     Rashid Ali Abdallah – CUF
  2. 3.    Chiku Aflah Abwao- Chadema
  3. 4.     Saluim Ali Mbarouk – CUF
  4. 5.    Salum Khalfam Barwany –  CUF
  5. 6.     Deo Haule  Filikuchombe- CCM
  6. 7.    Pauline Philipo Gekul- Chadema
  7. 8.    Asaa Othman  Hamad- CUF
  8. 9.     Prof.Kuliyokela Kahigi- Chadema
  9. 10.    Naomi  Mwakyoma Kaihula – Chadema
  10. 11.     Sylvester Kasulumbayi- Chadema
  11. 12.     Raya Ibrahim Khamis  - Chadema
  12. 13.     Mkiwa Hamad Kiwanga  -  CUF
  13. 14.     Susan  Limbweni Kiwanga- Chadema
  14. 15.     Grace Sindato Kiwelu –Chadema
  15. 16.     Kombo Khamis Kombo – cuf
  16. 17.     Joshua  Samwel  Nassari – Chadema
  17. 18.     Tundu Antiphas Lissu- Chadema
  18. 19.     Aphaxar  Kangi Lugola- CCM
  19. 20.    Susan Anselim Lymo- Chadema
  20. 21.     Moses Machali – NCCR Mageuzi
  21. 22.     John Shibuda Magalle – Chadema
  22. 23.    Faki  Haji  Makame-  CUF
  23. 24.     Esther Nicholas Matiko- Chadema
  24. 25.     Joseph Osmund Mbilinyi- Chadema
  25. 26.    Freman  Aikaeli Mbowe- Chadema
  26. 27.    Kurudhum Jumanne Mchuchuli – Chadema
  27. 28.     Halima James Mdee-Chadema
  28. 29.    John John Mnyika- Chadema
  29. 30.     Augustino Lyatonga Mrema- TLP
  30. 31.     Maryam Salum  Msabaha- Chadema
  31. 32.     Peter Msingwa-chadema
  32. 33.    Christowaja Gerson Mtinda- Chadema
  33. 34.     Philipa Geofrey Mturano- Chadema
  34. 35.    Christina Lissu Mughwai- Chadema
  35. 36.    Joyce John  Mukya – Chadema
  36. 37.    Mchungaji  Israel  Yohane  Natse – Chadema
  37. 38.    Philemon Ndesamburo- Chadema
  38. 39.     Ahmed  Juma Ngwali-  CUF
  39. 40.    Vincent  Josephat  Nyerere- Chadema
  40. 41.     Rashid  Ali Omar-  CUF
  41. 42.    Meshack  Jeremiah Opulukwa- Chadema
  42. 43.     Lucy Philemon Owenya- Chadema
  43. 44.     Rachel Mashishanga- Chadema
  44. 45.     Mhonga Said Ruhwanya – Chadema
  45. 46.     Conchesta Rwamlaza – Chadema
  46. 47.    Moza Abedi  Saidy-  CUF
  47. 48.    Joseph  Roman Selasini – Chadema
  48. 49.     David Ernest  Silinde- Chadema
  49. 50.     Rose Kamili Sukum  - Chadema
  50. 51.     Cecilia Daniel Paresso- chadema
  51. 52.    Kabwe Zuberi Zitto- Kigoma Kaskazini
  52. 53.     Magdalena Sakaya –  CUF
  53. 54.     Rebecca Mngodo-  CUF
  54. 55.     Sabreena Sungura -Chadema
  55. 56.    Hamad Rashid Mohammed- CUF
  56. 57.    Rukia Kassim Ahmed- CUF
  57. 58.    Mustapha Boay Akoonay -Chadema
  58. 59.     Abdalla Haji Ali -CUF
  59. 60.    Khatibu Said Ali -CUF
  60. 61.     Hamad Ali Hamad -CUF
  61. 62.      Riziki Omar Juma -CUF
  62. 63.     Haji Khatibu  Kai -CUF
  63. 64.     Anna Marystella John Malack -Chadema
  64. 65.     Hamad Rashid Mohamed  -CUF
  65. 66.     Rajab Mbarouk Mohamed -CUF
  66. 67.     Thuwayba Idrissa Muhamed -CUF
  67. 68.      Masoud Abdallah Salum -CUF
  68. 69.     Muhamad Ibrahim Sanya -CUF
  69. 70.     Ali Khamis Seif -CUF
  70. 71.     Haroub Muhammed Shamis -CUF
  71. 72.     Amina Amour Nassoro -CUF

Taswira Za Ziara Ya Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Huko Kusini Pemba



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Tangi la Maji la Ziwani Wilaya ya Chake chake Pemba, akiwa katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya kijamii ya Mkoa wa Kusini Pemba jana
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi ambao ni Wajumbe wa Kikosi cha (Task Force), ya Taifa kuhusu uvunaji wa zao la karafuu,alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa mamlaka ya Maji,alipowasili Ziwani katika ufunfuzi wa tangi la Maji katika shehia hiyo,akiwa katika ziara ya kutembelea miradi mbali mbali  ya kijamii ya Mkoa wa Kusini Pemba jana
Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Thuwaiba Edington Kisasi,akimkabidhi zawadi Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,ya tunzo ya karafuu ya mwaka 2011-2012,katika mkutano wa ufungaji wa msimu wa zao la Karafuu,hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Kikosi kazi cha (Task Force) ya Taifa kilichoshuhulikia uvunaji na uuzwaji wa zao la karafuu,katika ukumbi wa  Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,Rais aliufunga Msimu wa zao hilo kwa mwaka 2011-2012 jana,akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi kazi (TaskForce) ya taifa kuhusu uvunaji wa zao la karafuu huko kiwanda cha Makonyo Wawi ,Wilaya ya Chakechake Pemba , akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba jana.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar

Check vimwana Wa Miss Ukonga Wakijifua



Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la kumsaka Malikia wa Kitongoji cha Ukonga jijini Dar es Salaam wakiwa katiika picha ya pamoja wakati wakiendelea na mazoezi yao ya kujiandaa na shindano hiklo jana. Shindano la Miss Ukonga linataraji kufanyika Mei 5,2012 katika ukumbi wa Wenge Garden-Ukonga Mombasa. 
Baadhi ya warembo wanaoshiriki shindano la Miss Ukonga 2012 wakimsikiliza msanii nguli wa Filamu na Maigizo nchini, Single Mtambalike "Rich Rich" wakati alipokuwa akizungumza nao jana katika kambi yao ya mazoezi jijini Dar es Salaam.Shindano la Miss Ukonga linataraji kufanyika Mei 5,2012 katika ukumbi wa Wenge Garden-Ukonga Mombasa.Picha na Habari zimeletwa na  Mroki Mroki

Sasa Spika Wa Bunge Anne Makinda Akubali Kuwasilishwa Kwa Hoja ya Wabunge Kupiga Kura ya Kutokuwa na imauni na Waziri Mkuu Siku ya Jumatatu Bungeni Mjini Dodoma

Mbunge wa Singida Mashariki(CHADEMA) Mh. Tundu Lissu
---
Muda mfupi kabla ya kumalizika kikao Cha Bunge jioni ya leo mjini Dodoma,Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu alisimama kutaka muongozo wa Spika kuhusu Suala linaloendelea kwenye Bunge hilo la kukusanya Saini za wabunge wapatao 70 ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Mh. Lissu alisema kuwa kitendo cha Spika kutoa uamuzi kwa jambo ambalo halijamfikia mezani kwake ni kama ukiukwaji wa kanuni na sheria za Bunge na itaonyesha kuwa kuna majibu yanaandaliwa kwa hoja ambayo hatakuiona bado hajaiona na kwa kufanya hivyo nikukiuka taratibu.

Baada ya Mh.Lissu kutaka muongozo huo,Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda alisema kuwa hajasema kwamba suala hilo si halali kufanyika ila alichosema halitawezekana kwa kikao hiki cha Bunge,kwa sababu linamalizika siku ya Jumatatu (23 April,2012), kwahiyo itakuwa ni vigumu sana kulifanya jambo hilo ndani ya Kikao cha Bunge hili.

Aidha akitoa ufafanuzi zaidi Mh. Spika mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo,Mh. John Mnyika,kusimama na yeye akitaka muongozo juu ya jambo hilo hilo ambapo alihoji kwamba,kuna tatizo gani kama watu wakiendelea kusaini (saini ambazo Mh. Mnyika alisema idadi yake imefikia 66 ) na kuwasilisha hoja siku ya jumatatu kwaajili ya kujadiliwa Bunge lijalo?

Mh. Anne Makinda alisema kwamba yeye hajasema kwamba jambo hilo halifai, "Naomba nieleweke na answered zitaletwa,sasa hivi nilicho kisema! nikwamba suala hilo haliwezekani kwa Bunge hili kwakuwa jumatatu ndio linafikia kikomo lakini kama mtaleta kwa kikao kijacho hakuna tatizo" alisema Makinda.

Taswira Za Yale Maandamano Ya Wanaharakati Wanaodai Kura ya Maoni Dhidi ya Muungano Zanzibar

Mdau wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muunganoakisindikizwa na polisi kuondoka sehemu ya maandamano
Kiongozi wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muungano Rashid Salum Adiy akizungumza muda mfupi baada ya kushikwa na polisi kwa kufanya maandamano kinyume na sheria
Kiongozi wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muungano Rashid Salum Adiy akizungumza na simu.
Jeshi la Polisi likitoa tahadhari kwa wananchi waliofika katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni juu ya Muungano
Kikosi maalum cha Polisi cha kuzuia fujo kikijipanga kukabiliana na wanaharakati waliofika baraza la Wawakilishi jana
Baadhi ya Wanaharakati waliokuwepo kwenye viwanja vya baraza la wawakilishi wakisubiri hatima yao ya kutaka kuonana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho.
Hashim na wenzake wakiwa katika gari la Jeshi la Polisi likiwachukua na kuwapeleka Madema, baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni itakayoamua kuwepo au kutokuwepo Muungan.Picha na Habari na Mdau Othman Maulid