Tuesday, May 29, 2012

Mustafa Sabodo Atoa Billioni 5 Kwa Ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuegesha Magari Jijini


 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akimkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo vibali vya ujenzi wa jengo hilo, kushoto ni  Mwenyekiti wa Madhehebu  ya Khoja Shia Shiraz Walji
--
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya sh.bilioni 5 kwa madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya kujenga jengo la maegesho ya magari.
 
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
 
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
 
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya magari katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa jengo hilo la kwanza kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
 
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema Silaa.
 
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio maana imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
 
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
 
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote.

Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) Atinga Mahakama Kuu



Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiwa amezungukwa na walinzi kwenye Mahakama Kuu Dar es Salaam jana kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuhusishwa na kifo cha msanii mwenzake Steven Kanumba.Na Mpigapicha Wetu

TASWIRA ZA SIMBA SC WALIVYOSHEREHEA UBINGWA WAO DAR LIVE



 Baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao wakati wakipita katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam jana.
 Mashabiki na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika  msafara kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live kusherehekea ubingwa wa timu yao jana.
Wachezaji na viongozi wa Simba wakifungua shampeini wakati wakisherehekea ubingwa wao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana.
 Naibu Waziri Amos Makala akimvisha medali Uhuru Selemani.
 Meneja wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja shilingi milioni 3 zilizotolewa na Dar Live kama pongezi kwa timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012.
Wachezaji wa Simba wakipata menyu pembeni ya kombe lao.
 Baadhi ya mashabiki waliohudhuria sherehe hizo.
 Wachezaji na viongozi wa timu ya Simba wakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (katikati aliyeshika kombe).
Mashabiki wa Simba wakiingia ndani ya Ukumbi wa Dar Live tayari kwa sherehe za ubingwa.
---
TIMU ya Simba SC ya jijini Dar jana ilisherehekea ubingwa wake wa 2011/2012 pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa burudani wa DAR LIVE. Sherehe hizo zilitanguliwa na msafara wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu ambao walianzia safari yao makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi  na kupitia mitaa kadhaa ya jiji kabla ya kumalizikia katika ukumbi wa Dar Live. Katika msafara huo wachezaji wa Simba walikuwa katika lori la wazi lililopambwa bendera na vitambaa vya rangi nyekundu na nyeupe huku wakiwa na kombe lao walilolibeba

Kama Kawaida Daily Mail Latoa Taswira Za Majangili Jinsi Wanavyokatili Wanyama Mbuga ya Mikumi

 Weak: The animal was so sick it struggled to raise its head as park wardens approached
 Lucrative: Many of the snares are set by poachers who then butcher the animals for their parts which are used in traditional Chinese medicine
 Desperately injured: The young male lion cub was spotted in Mikumi National Park in Tanzania with a poacher's snare twisted cruelly round his neck
 Doomed to die: The wire was twisted so tight that the lion was unable to eat
The final journey: The lion slopes off into the long grass of the park where he would soon die either of starvation or infection
--
Wire snare caught so tightly around his neck he cannot eat, this young male lion is doomed to die a slow and agonising death.Within a matter of days he will be lying in the African bush gasping his last breath.

Nor is he alone in his grim fate. The sight is increasingly common in parts of the continent when a growing number of lions have fallen victim to poaching.Kwa Habari zaid

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA):'' Tunaomba Waislamu Wote Kurudi Majumbani na Kuendelea na Shughuli Zao za Kawaida za Maisha na Wasijihusishe na Kitendo Chochote Cha Uvunjifu wa Amani Maimamu wote Tunaomba Wawatake Waumuni Wao Kutunza Amani Kama Mafundisho ya Dini Yetu Yanavyotuelekeza ''.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) Muhiddin Zubeir Muhiddin


Watukufu waislam,
Assalamu Alykum Warahmatullah Wabarakatu.
Kwanza kabisa tunataunguliza shukurani kwa Allah (S.W) kwa uwezo wake kutuwezesha kuishi katika visiwa hivi kwa salama na amani licha ya kupita katika mikiki mbali mbali. Aidha sala na salamu zimfikie Mtume Muhammad (S.A.W), Mtume ambaye ametufundisha dini ya amani inayotutaka kuishi kwa amani, mapenzi na umoja katika jamii.
 
Watukufu Waislam,
Kufuatia kukamatwa kwa Sheikh Mussa Juma ambaye ni muhadhiri wa dini ya kiislam hapo jana tarehe 26/05/2012 kumejitokeza vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyodaiwa kufanywa na watu wanaotaka kuachiwa kwa sheikh huyo sambamba na matumizi ya nguvu ya jeshi la polisi kukabiliana na watu hao, hali ambayo imesababisha kuvunjika kwa amani, watu kuishi kwa taharuki, khofu kutawala katika jamii, kusita kwa shughuli za maisha kwa wakazi wa Manispaa ya Mjini Unguja pamoja na kusababisha matatizo ya usafiri katika manispaa hiyo.

Katika muktadha huu Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) inawataka waislamu wote kurudi majumbani na kuendelea na shughuli zao za kawaida za maisha na wasijihusishe na kitendo chochote cha uvunjifu wa amani. Maimamu wote tunaomba wawatake waumuni wao kutunza amani kama mafundisho ya dini yetu yanavyotuelekeza. Sambamba na hili maimamu waendelee kuiombea dua nchi kudumu katika usalama na amani.

JUMAZA inawataka waumuni wote wafahamu kuwa kuhusu watu waliokamatwa na kuzuiliwa na jeshi la polisi mpaka sasa, viongozi wa taasisi wa Jumuiya za kiislamu wanafanya kila juhudi kuzungumza na viongozi wa kitaifa na jeshi la polisi katika kulitafutia ufumbuzi suala lililojitokeza na hatua yoyote itakayofikiwa waislamu watajuilishwa.

Wabilahi Tawfiq
Imeandaliwa na;
Muhidin Zubeir Muhidin
Katibu Mtendaji wa JUMAZA

MBUNGE WA MBEYA MJINI(CHADEMA)JOSEPH MBILINYI ‘SUGU’ KUTOA BURUDANI KALI DAR LIVE JUMAPILI HII

Mr II akiongea na waandishi wa habari juu ya onyesho hilo.

Mr II akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari juu ya onyesho hilo.
 Mratibu wa Burudani na Matukio Dar Live, Juma Mbizo (kushoto) akiwa na Mr II.

Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdalah Mrisho (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu burudani itakayotolewa na Sugu akiwa na wasanii wengine wakali   ambao ni pamoja na Professor J na Juma Nature.  Kulia ni Mratibu wa Shoo za Wasanii Dar Live, Luqman Maloto.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza mkali huyo.

Check:Taswira Zaidi Ya Jinsi Mambo Yalivyokua Huko Zanzibar