Thursday, May 10, 2012

CHECK ALICHOKISEMA OBAMA JUU YA MAHUSIANO YA JINSIA MOJA

Rais Barack Obama amesema kwamba watu wa jinsia moja wawe na haki ya kuoana.
Bwana Obama amesema daima amekuwa mgumu kukubali kwamba wanaume na wanawake wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja nchini Marekani watendewe haki na jamii kwa kutambua uhusiano huo, lakini amekuwa akipitia kile anachokiita mabadiliko ya kimtazamo kuhusu suala la ndoa za jinsia moja.
Kwa kauli hii Obama anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuunga mkono ndoa za jinsia moja, suala ambalo limeleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa Marekani. Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa Wamarekani kuhusu kuunga mkono ndoa za aina hii.
Rais Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani kwa muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao wamejikita katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.
Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.
Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.
Amesema wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za jinsia moja.
Kauli ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa ni muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke

Wednesday, May 9, 2012

CHECK Mapigano kuanza upya libya

Maafisa wawili wa usalama nchiniLibya wameuawa baada ya waasi wa zamani kushambulia ofisi ya Waziri Mkuu mjini Tripoli.
Mtu aliyeshudia alisema magari aina ya pick-up yenye kubeba makombora yalilizunguka jengo hilo na mapigano yakaanza.
Msemaji wa serikali baadaye alisema mapigano yamekoma.
Mashambulizi yanaarifiwa kufanywa na waasi wa zamani waliopigana kumuondoa madarakani Kanali Gaddafi mwaka uliopita ambao wanadai malipo yao walioahidiwa kupewa kwa utaratibu wa maalum.
Watu wengi waliokuwemo katika jengo hilo walikimbia akiwemo Waziri wa Fedha na Naibu Waziri Mkuu.

'Risasi kutokea ndani'

Ashur Shamis, mshauri wa habari wa Waziri Mkuu Abdurrahim al-Keib, aliiambia BBC kuwa waziri mkuu na maafisa kadhaa walikuwa salama na kwamba mapigano yaliyodumu kwa saa kadhaa yalikwisha.
Walioshuhudia walisema mashambulizi yalifanywa na wanamgambo kutoka Yafran, mji uliojaa wafuasi wa kundi la kikabila la Berber lililo umbali wa kilometa 100 (maili 60 ) kusini magharibi mwaTripoli.
Haijulikani Waziri mkuu Abdurrahim al-Keib aliko.
"Watu wengi waliolizunguka jengo hilo walilifyatulia risasi wakiwa na silaha za makombora," mfanyakazi wa serikali aliiambia AFP. "Baadhiyao waliingia katika jengo hilo na kuanza kufyatua risasi ndani," aliongeza.
Afisa mmoja wa wizara ya ndani alisema takriban askari wawili wa usalama waliuawa na wengine kujeruhiwa katika mapigano hayo.
Mwandishi wa BBC Rana Jawad mjini Tripoli anasema pamoja na kupatiwa fedha, waasi hao wanadai wale waliojeruhiwa wakati wa mapinduzi mwaka jana wamepewe matibabu nje ya nchi.
Mpango wa malipo ulisitishwa mwezi uliopita huku kukiwa na tuhuma za udanganyifu.
Mwandishi wetu anasema jengo hilo si mara ya kwanza kwa kushambuliwa, hili ni la pili katika kipindi cha miezi miwili, lakini mara hii kuna nguvu zaidi.
Serikali ya Libya imekuwa ikijaribu kuwashawishi mamia ya wanamgambo walioshika silaha dhidi ya Kanali Gaddafi kuzisalimisha huku kukiwa na wasiwasi kuhusu usalama.

Tuesday, May 8, 2012

Mkapa atoa ushahidi mahakamani

Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa afika mahakamani kutoa ushahidi
Rais Mstaafu Tanzania Benjamin William Mkapa amefika mbele ya mahakama akiwa ni shahidi wa kwanza upande wa utetezi katika mashataka yanayomkabili aliyewahi kuwa balozi waTanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiongozi aliyewahi kushika madaraka makubwa nchiniTanzaniakufika mbele ya mahakama akitakiwa kutoa ushahidi upande wa utetezi dhidi ya ya tuhuma zinamzomkabili mmoja wa watumishi katika kipindi cha utawala wake.
Katika Mahakama ya hakimu mkazi ya kisutu iliyojaa watu wengi Rais huyo mstaafu mara baada ya kuapa ameieleza mahakama kuwa serikali yake ilifahamu na kisha kuridhia ununuzi wa nyumba au jengo la ubalozi waTanzania nchini Italia baada ya kushauriana na Balozi waTanzanianchini Italia wakati huo Profesa Costa Mahalu.
Hatua hiyo ilifuatia kuthaminiwa kwa jengo lenyewe kulikofanywa na Mamlaka husika kutoka serikali yaTanzania. Baadaye jengohilolilinunuliwa na Bw Mkapa kulizidnua rasmi alipokuwa ziarani kikazi nchini Italia Mwezi February mwaka 2003.
Akijibu swali la wakili upande wa mashtaka ni kwa nini malipo ya shilingi Bilioni mbili na milioni 900 yakafanyika kwa kupitia akaunti mbili tofauti,Bwana Mkapa ameiambia mahakama hiyo kuwa alijulishwa kuwa hilo lilikuwa sharti na muuzaji nyumba na hivyo kwa upande wa serikali hakuona kama kuna tatizo akizingatia kuwa thamani ya jengo iliishafanywa na kuwaridhisha wao kama serikali huku kukiwa na mahitaji makubwa ya Serikali ya Tanzania kuwa na majengo ya kudumu ambayo yangemilikiwa na serikal.
Mmoja wa mawakili ambaye alimuongoza Bwana Makapa kutoa ushahidi wake Wakili Alex Mgongolwa alimweleza mwandishi wa BBC Eric Nampesya mjini Dar es salaam kuwa amefurahia kumuongoza Bwana Mkama kutoa ushahidi wake mahakamani. Alisema ‘kitendo cha Rais mstaafu kufika mahakamani kama shahidi kwa upande mwingine kimeonyesha ni jinsi gani misingi ya sheria inaheshimiwa wakiwemo kiongozi wastaafukamaBwana Benjamin Mkapa.’
Bw Mkapa akiwa na viongozi wengine wa Afrika
Kiongozi huyo anakuwa wa kwanza katika historia yaTanzaniakwa miaka zaidi ya hamsini kwa kiongozi aliyewahi kuwa Rasi kufika mbele ya mahakama na kutoa ushahidi.
Katika kesi hiyo Balozi huyo wa zamani wa Tanzania nchini Italia Profesa Costa Mahalu anashtakiwa kwa kuhujumu uchumi ambapo inadakiwa kuwa alitoa taarifa za uongo kuhusu bei halisi ya jengo la ubalozi lililonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa kutaja bei ya juu, ikiwa ni tofauti na bei yake halisi.
Prof Costa Mahalu anadaiwa kuisababishia serikali ya Tanzania hasara ya $ 3.098 milioni (shilingi bilioni 2 na milioni 900 za Tanzania).
                                   KWA HISANI YA BBC-SWAHILI

Sunday, May 6, 2012

check CHADEMA yailiza CCM,ma elfu warudisha kadi..

Home

 Send to a friend

Umati wa wananchi waliofurika wakisikiliza hotuba za viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema)kwenye uwanja wa NMC mjni Arusha jana,viongozi mbalimbali na wanachama wa CCM walijiunga rasmi na Chadema.Picha na Filbert Rweyemamu
MBOWE ASEMA MAWAZIRI 7,WABUNGE 70 WAOMBA KUJIUNGA,10,000 WAKABIDHIWA KADI ARUSHA
Peter Saramba, Arusha
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema kuna zaidi ya wabunge 70 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), wameomba kujiunga na chama hicho cha upinzani.

Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya NMC, Unga Ltd, jijini Arusha jana, Mbowe alisema katika orodha hiyo, wamo mawaziri saba waliotajwa katika Baraza lililotangazwa juzi na Rais
Jakaya Kikwete.

“Sasa wanaowataja akina Ole Millya, Bananga na wengine watashangaa kusikia orodha na majina ya wana CCM watakaojiunga Chadema,” alisema Mbowe.

Alitumia mkutano huo kuwatoa hofu wana Chadema wanaotilia shaka wimbi la viongozi na wana CCM wanaojiengua na kujiunga na chama hicho kikuu cha upinzani kuwa Chadema iko imara na hakiwezi kuhujumiwa wala kupenyezewa mamluki kama baadhi wanavyodhani.

Mbowe alitamba kuwa ameongoza harakati za upinzani kwa zaidi ya miaka
20 sasa ambayo imeanza kuzaa matunda kwa Watanzania kukiamini Chadema hivyo hawezi kukubali kuruhusu mtu yeyote yule anayetumia njia ya wazi au ya kificho kukidhoofisha.

“Kuna watu walipata hofu na kunitumia hadi sms kuhoji iwapo akina Ole Millya wametumwa na Lowasa (Edward Lowasa, Mbunge wa Monduli) kuja kukipeleleza Chadema, najua baadhi mko hapa na ninawatoa hofu kuwa
chama chetu ni taasisi imara isiyoweza kuhujumiwa na mtu au kundi la watu kwa nguvu wala mbinu yoyote,” alitamba Mbowe.

Aliwataka wanaofikiri Lowassa na wengine wenye ukwasi kuweza kununua viongozi wa Chadema kujiuliza kwanini hawakuweza kufanya hivyo kipindi chote walichokitumia kukijenga chama hicho ambacho ni tishio kwa CCMna mafisadi wote nchini.

Mbowe alitumia fursa hiyo kuponda uteuzi wa Baraza la Mawaziri akisema Rais Kikwete amevunja katiba kwa kuwateua watu ambao hawajaapishwa kuwa wabunge kushika nafasi za uwaziri.

Licha ya kuvunja katiba kwenye uteuzi, Rais pia amekiuka kwa kuwateua Wazanzibari kwenye wizara ambazo siyo za Muungano kama Afya aliyokabidhiwa na Dk Husein Mwinyi.


Makada wapokewa

Waliokuwa makada wa CCM waliojiengua na kuhamia Chadema walipokelewa na wote kuahidi kutumia uzoefu, juhudi na maarifa yao kisiasa kukijenga chama chao kipya kwa kushirikiana na wanachama na viongozi
wote.

Ole Millya aliahidi kudhihirisha kuwa hakua mzigo CCM kama wanavyodai baadhi ya viongozi mara alipotangaza kujiunga upinzani kwa kukifanyia chama hicho kitu ambacho hakitasahaulika milele akianzia na kuipenyeza
Chadema kwa jamii ya Wamaasai.

“Vijana wengi walioko ndani ya CCM wanaishi kwa matumaini ya kupewa vyeo kama ukuu wa wilaya na nyadhifa mbalimbali badala ya kusimamia haki na ustawi wa taifa,” alisema Ole Millya

Mila na laana kwa Ole Millya akigeuka

Kabla ya viongozi kuanza kuhutubia, wazee wa kimila wa jamii ya Wamaasai waliendesha sala ya Mila hiyo kwa kumkalisha kwenye kigoda Ole Millya na kumpa laani iwapo atageuka na kukisaliti Chadema.

“Mungu amekutuma wewe Ole Millya kuwakomboa Wamasaai kutoka kwenye utumwa waliokaa nao kwa miaka 50 kama ambavyo alimtuma Mussa kuwakomboa Waisraeli kutoka kwenye utumwa wa miaka 40 Misri. Usiwe
kinyonga kwa kugeuka, angalia huu umati ulioko mbele yako,” alisema Mzee Naftali Mollel

Kwa upande wao aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sombetini, Alphonce Mawazo na Ally Banganga aliyekuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM waliojiunga Chadema walisema chama hicho tawala tayari imekufa na kinasubiri kuepelekwa chumba cha kuhifadhia maiti kusubiri mazishi.

“Wanaohoji kwanini tumetoka CCM kwanza watueleze hicho chama kilipo kwa sababu tayari kimekufa mioyoni mwa wa Watazanania,” alisema Mawazo huku akishangiliwa

Akihutubia mkutano huo uliohudhuriwa na umati mkubwa wa wananchi, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema aliwataka wanaCCM wanaotaka kukihama chama hicho na kujiunga Chadema kufanya haraka kwa
sababu mlango wa ‘neema’ unakaribia kufungwa.

“Kuna kipindi kinakuja siku siyo nyingi ambapo kujiunga Chadema itakuwa dili. Wanaotaka kuja na wafanye hivyo sasa kabla hatujafunga milango,” alisema Lema

Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, alisema moto uliowashwa na Operesheni ‘Vua gamba, vaa gwanda’ ulioanzia Arusha, sasa umeanza kuenea nchi nzima akitaja matukio ya madiwani na wanachama
kadhaa kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa kuhamia Chadema.

Golugwa alisema baada ya mkutano wa jana Jijini Arusha, mikutano ya Operesheni ya  Movement for Change inahamia wilaya za Longido, Ngorongoro, Simanjiro na kumalizikia Monduli.

Katika mkutano huo, Mbowe alikabidhi kadi za uanachama kwa Ole Millya, Bananga, Mawazo na viongozi kadhaa wana CCM waliojiunga Chadema ambapo kwa niaba ya wenzao.

Hamasa kubwa iligubika umati uliohudhuria baada ya mwana CCM mwenye asili ya kiasia aliyejitambulisha kwa jina la Adil Dewji alipopanda jukwani kurejesha kadi ya CCM na kujiunga Chadema.

Wengine waliojiunga Chadema kutoka CCM ni pamoja na wenyeviti kadhaa wa Serikali za mitaa kutoka Wilaya za Arusha, Monduli, Arumeru, Ngorongoro na Longido ambao waliwakilishwa na Ignas Mfinanga aliyekuwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Themi, jijini Arusha.

Check Dege La Jeshi Lililotorosha Twiga Wetu!



"MIONGONI MWA UFISADI ULIOTIA FORA TANZANIA EBWANA HUU ULIPITA MIPAKA. HII NI NDEGE YA JESHI LA ANGA LA QATAR AMBAYO ILITUMIKA KUIBIA WANYAMA 130 WA AINA 14 TOFAUTI NCHINI TANZANIA NA KUWAPELEKA DOHA QATAR. SASA WATANZANIA WENZANGU NAWAULIZA, INAMAANA WAHUSIKA WALI-PLAN KUA KABISA SOKO LA UTALII TANZANIA? MI NAMASHAKA SANA NA UPEO WA FIKRA KWA BAADHI YA VIONGOZI WETU.
KWA HISANI YA HAKI-NGOWI 

Friday, May 4, 2012

CHECK ORODHA YA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WALIOTEULIWA NA RAIS LEO



ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI
1.            OFISI YA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,
2.            OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H.  Suluhu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,
3.            OFISI  YA WAZIRI MKUU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri  Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,
4.            WIZARA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,
Waziri wa Ujenzi
Dr.  John P. Magufuli, Mb.,
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,
Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,
Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof.  Makame M. Mbarawa, Mb.,
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof.  Anna K. Tibaijuka, Mb.,
Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe,  Mb.,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,
Waziri wa  Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,
Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,
Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,
Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,
Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,
Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,
5.            NAIBU MAWAZIRI
 OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI
6.            OFISI YA MAKAMU WA RAIS
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,
7.            OFISI YA WAZIRI MKUU
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi  ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,
8.            WIZARA MBALIMBALI
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,
Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo  ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,
Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,
Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,
Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,
Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,
Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,
Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,
Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012
KWA HISANI YA HAKI-NGOWI

Wednesday, May 2, 2012

Check.FERI YAZAMA INDIA NA KUUWA WATU 103

Takriban watu 103 wanahofiwa kufariki baada ya feri walimokuwa wakisafiria kugongwa na dhoruba Kaskazini Mashariki mwa India.
Polisi wamethibitisha taarifa hiyo.
Taarifa zinasema kuwa feri hiyo ilikuwa imewabeba abiria 300 wakati ilipopinduka kwenye Mto Brahamaputra katika jimbo la Assam.
Taarifa zinasema kuwa watu 100 hawajulikani waliko na kwamba wengine waliokolewa au kujisilimisha baada ya kupinduka kwa feri hiyo.
Kutokana na hali mbovu ya feri nyingi katika eneo hilo kumekuwepo ajali nyingi lakini ajali hii ni mojawapo mbaya zaidi kuwahi kutokea hivi karibuni katika eneo hilo.
Maafisa wa polisi wamesema kuwa ajali hiyo ilitokea katika Wilaya Dhubri kufuatia kimbunga kikali.
Dhubri ni karibu kilomita 350 kutoka mji mkuu wa Jimbo la Assam wa Guwahati.
Polisi walisema feri hiyo ilivunjika vipande viwili kutokana na kimbunga hicho.
"niliona watu wakisombwa na maji kwa kuwa maji yalikuwa yakienda kwa kasi sana," mtu mmoja aliyeshuhudia ajali, Rahum Kamarkar aliambia shirika la habari la AFP.