Sunday, June 10, 2012

ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE: MH. BOB MAKANI WA CHADEMA AFARIKI DUNIA


                               Mwanasiasa maarufu,  mwasisi, katibu mkuu wa kwanza na mwenyekiti wa pili  wa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) amefariki dunia hii leo, msiba upo nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach, karibu na Rainbow.  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI.

ZILIZOTUFIKIA PUNDE: PROFESA GEORGE SAITOTI AFARIKI DUNIA


WAZIRI WA MAMBO YA NDANI NA MBUNGE WA NGONG, NCHINI KENYA  AMEFARIKI DUNIA SAA TATU ASUBUHI YA LEO JUMAPILI KWA AJALI YA HELICOPTER AKIWA SAFARINI KUELEKEA JIMBONI(NDHIWA) KWA MBUNGE ORWA OJODE AMBAYE PIA AMEFARIKI KATIKA AJALI HIYO , PAMOJA NA WATU WENGINE WATANO WALIOKUWEMO KATIKA MSAFARA HUO. MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI. AMEN...source daily nation

Sunday, June 3, 2012

Mubarak ahukumiwa kifungo cha maisha


Rais wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, amehukumiwa kifungo cha maisha na mahakama mjini Cairo.
Alikutikana na hatia ya kuhusika na mauaji ya waandamanaji wakati wa ghasia zilizopelekea yeye kutolewa madarakani mwaka jana.
Hakimu Ahmed Refaat alisema watu wa Misri walivumilia miaka 30 ya dhiki chini ya utawala wa Bwana Mubarak, lakini kesi ilikuwa ya haki.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi wa zamani, Habib Al Adly, naye piya amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kuhusika na mauaji ya waandamanaji.
Baada ya hukumu kutolewa kulizuka mtafaruku mahakamani wakati makundi yanayopingana yalipoanza kupigana.

MFANO WA KUIGWA: Rais Banda auza ndege ya rais


 
Rais wa Malawi, Joyce Banda, ameamua kuuza ndege ya rais pamoja na magari 60 ya kifahari.
Ndege hiyo ilinunuliwa kwa dola milioni-13 na rais aliyemtangulia, Bingu wa Mutharika, aliyefariki mwezi wa Aprili.
Rais Banda amenukuliwa kusema kwamba anatosheka kusafiri kwenye ndege za abiria kama watu wengine, kwa sababu ameshazowea kutembea kwa miguu na kusaidiwa na wasafiri njiani.
Fedha zitazopatikana katika mauzo ya ndege na magari hayo, zitatumiwa kuwasaidia maskini wa Malawi.
Serikali ya Uingereza, ambayo ndio mfadhili mkubwa wa koloni yake hiyo ya zamani, imepokea vema uamuzi huo kuwa ni ishara inayotia moyo.

Tuesday, May 29, 2012

Mustafa Sabodo Atoa Billioni 5 Kwa Ajili ya Ujenzi wa Jengo la Kuegesha Magari Jijini


 Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akimkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodo vibali vya ujenzi wa jengo hilo, kushoto ni  Mwenyekiti wa Madhehebu  ya Khoja Shia Shiraz Walji
--
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya sh.bilioni 5 kwa madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya kujenga jengo la maegesho ya magari.
 
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
 
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
 
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya magari katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa jengo hilo la kwanza kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
 
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema Silaa.
 
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio maana imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
 
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
 
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote.

Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) Atinga Mahakama Kuu



Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiwa amezungukwa na walinzi kwenye Mahakama Kuu Dar es Salaam jana kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuhusishwa na kifo cha msanii mwenzake Steven Kanumba.Na Mpigapicha Wetu

TASWIRA ZA SIMBA SC WALIVYOSHEREHEA UBINGWA WAO DAR LIVE



 Baadhi ya wachezaji wa Simba SC wakishangilia pamoja na kombe lao wakati wakipita katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam jana.
 Mashabiki na wapenzi wa Simba SC wakiwa katika  msafara kuelekea katika Ukumbi wa Dar Live kusherehekea ubingwa wa timu yao jana.
Wachezaji na viongozi wa Simba wakifungua shampeini wakati wakisherehekea ubingwa wao ndani ya ukumbi wa Dar Live jana.
 Naibu Waziri Amos Makala akimvisha medali Uhuru Selemani.
 Meneja wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi nahodha wa Simba SC, Juma Kaseja shilingi milioni 3 zilizotolewa na Dar Live kama pongezi kwa timu hiyo kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2011/2012.
Wachezaji wa Simba wakipata menyu pembeni ya kombe lao.
 Baadhi ya mashabiki waliohudhuria sherehe hizo.
 Wachezaji na viongozi wa timu ya Simba wakiwa na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla (katikati aliyeshika kombe).
Mashabiki wa Simba wakiingia ndani ya Ukumbi wa Dar Live tayari kwa sherehe za ubingwa.
---
TIMU ya Simba SC ya jijini Dar jana ilisherehekea ubingwa wake wa 2011/2012 pamoja na mashabiki wake katika ukumbi wa burudani wa DAR LIVE. Sherehe hizo zilitanguliwa na msafara wa magari, pikipiki na watembea kwa miguu ambao walianzia safari yao makao makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi  na kupitia mitaa kadhaa ya jiji kabla ya kumalizikia katika ukumbi wa Dar Live. Katika msafara huo wachezaji wa Simba walikuwa katika lori la wazi lililopambwa bendera na vitambaa vya rangi nyekundu na nyeupe huku wakiwa na kombe lao walilolibeba