Tuesday, May 29, 2012

Kama Kawaida Daily Mail Latoa Taswira Za Majangili Jinsi Wanavyokatili Wanyama Mbuga ya Mikumi

 Weak: The animal was so sick it struggled to raise its head as park wardens approached
 Lucrative: Many of the snares are set by poachers who then butcher the animals for their parts which are used in traditional Chinese medicine
 Desperately injured: The young male lion cub was spotted in Mikumi National Park in Tanzania with a poacher's snare twisted cruelly round his neck
 Doomed to die: The wire was twisted so tight that the lion was unable to eat
The final journey: The lion slopes off into the long grass of the park where he would soon die either of starvation or infection
--
Wire snare caught so tightly around his neck he cannot eat, this young male lion is doomed to die a slow and agonising death.Within a matter of days he will be lying in the African bush gasping his last breath.

Nor is he alone in his grim fate. The sight is increasingly common in parts of the continent when a growing number of lions have fallen victim to poaching.Kwa Habari zaid

Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA):'' Tunaomba Waislamu Wote Kurudi Majumbani na Kuendelea na Shughuli Zao za Kawaida za Maisha na Wasijihusishe na Kitendo Chochote Cha Uvunjifu wa Amani Maimamu wote Tunaomba Wawatake Waumuni Wao Kutunza Amani Kama Mafundisho ya Dini Yetu Yanavyotuelekeza ''.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) Muhiddin Zubeir Muhiddin


Watukufu waislam,
Assalamu Alykum Warahmatullah Wabarakatu.
Kwanza kabisa tunataunguliza shukurani kwa Allah (S.W) kwa uwezo wake kutuwezesha kuishi katika visiwa hivi kwa salama na amani licha ya kupita katika mikiki mbali mbali. Aidha sala na salamu zimfikie Mtume Muhammad (S.A.W), Mtume ambaye ametufundisha dini ya amani inayotutaka kuishi kwa amani, mapenzi na umoja katika jamii.
 
Watukufu Waislam,
Kufuatia kukamatwa kwa Sheikh Mussa Juma ambaye ni muhadhiri wa dini ya kiislam hapo jana tarehe 26/05/2012 kumejitokeza vitendo vya uvunjifu wa amani vinavyodaiwa kufanywa na watu wanaotaka kuachiwa kwa sheikh huyo sambamba na matumizi ya nguvu ya jeshi la polisi kukabiliana na watu hao, hali ambayo imesababisha kuvunjika kwa amani, watu kuishi kwa taharuki, khofu kutawala katika jamii, kusita kwa shughuli za maisha kwa wakazi wa Manispaa ya Mjini Unguja pamoja na kusababisha matatizo ya usafiri katika manispaa hiyo.

Katika muktadha huu Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) inawataka waislamu wote kurudi majumbani na kuendelea na shughuli zao za kawaida za maisha na wasijihusishe na kitendo chochote cha uvunjifu wa amani. Maimamu wote tunaomba wawatake waumuni wao kutunza amani kama mafundisho ya dini yetu yanavyotuelekeza. Sambamba na hili maimamu waendelee kuiombea dua nchi kudumu katika usalama na amani.

JUMAZA inawataka waumuni wote wafahamu kuwa kuhusu watu waliokamatwa na kuzuiliwa na jeshi la polisi mpaka sasa, viongozi wa taasisi wa Jumuiya za kiislamu wanafanya kila juhudi kuzungumza na viongozi wa kitaifa na jeshi la polisi katika kulitafutia ufumbuzi suala lililojitokeza na hatua yoyote itakayofikiwa waislamu watajuilishwa.

Wabilahi Tawfiq
Imeandaliwa na;
Muhidin Zubeir Muhidin
Katibu Mtendaji wa JUMAZA

MBUNGE WA MBEYA MJINI(CHADEMA)JOSEPH MBILINYI ‘SUGU’ KUTOA BURUDANI KALI DAR LIVE JUMAPILI HII

Mr II akiongea na waandishi wa habari juu ya onyesho hilo.

Mr II akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari juu ya onyesho hilo.
 Mratibu wa Burudani na Matukio Dar Live, Juma Mbizo (kushoto) akiwa na Mr II.

Meneja Mkuu wa Global Publishers Abdalah Mrisho (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu burudani itakayotolewa na Sugu akiwa na wasanii wengine wakali   ambao ni pamoja na Professor J na Juma Nature.  Kulia ni Mratibu wa Shoo za Wasanii Dar Live, Luqman Maloto.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza mkali huyo.

Check:Taswira Zaidi Ya Jinsi Mambo Yalivyokua Huko Zanzibar


Saturday, May 26, 2012

Mkutano wa Kujadili Maendeleo ya Matumizi ya Nishati Karne ya 21 Kwa Nchi za Afrika Wamalizika Nchini Afrika Kusini


 Pichani shoto ni Rais Mtsaafu wa Zanzibar,Mh Abeid Aman Karume akifafanua jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo uliohusu maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika
 Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano),akifafanua jambo kwa wageni waalikwa.
  Pichani juu ni wageni waalikwa mbalimbali waliofika kuhudhuri mkutano huo wa maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika
  Mmoja wa wageni waalikwa akichangia jambo.
  Wageni waalikwa wakifuatilia jambo wakati mkutano ukiwa unaendelea. 
 Wageni waalikwa mbalimbali wakihudhuria mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini .
 Pichani shoto ni Rais Mtsaafu wa awamu ya pili wa Tanzania,Mh Ally Hassan Mwinyi akiagana na Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano), mapema jana jioni,mara baada ya mkutano wa siku tatu uliohusu kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini .
Pichani shoto ni Rais Mtsaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh Benjamin Mkapa akiagana na Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania mapema jana jioni,mara baada ya mkutano wa siku tatu uliohusu kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini .
 Pichani shoto ni Rais Mtsaafu wa Zanzibar,Mh Abeid Aman Karume akiagana na Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano), mapema jana jioni,mara baada ya mkutano wa siku tatu uliohusu kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini
Wahariri wa vyombo vya habari kutoka nchini Tanzania,wakiagana na Marais Wastaafu wa Tanzania,mara baada ya mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini .
Pichani shoto ni Rais Mtsaafu  Nicéphore Dieudonné Soglo wa Benin akiagana na Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano), mapema jana jioni,mara baada ya mkutano wa siku tatu uliohusu kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini
 Kushoto ni Balozi Charles Stith  ambaye aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Tanzania (Mratibu mkuu wa mkutano),Rais Mtsaafu wa awamu ya pili wa Tanzania,Mh Ally Hassan Mwinyi pamoja na  Rais Mstaafu wa Zanzibar,Mh Abeid Aman Karume wakiwa katika picha ya pamoja jioni ya jana na Wahariri wa vyombo vya habari kutoka Tanzanania,mara baada kumalizika kwa mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini .
 Baadhi ya Wanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam (UDSM) wakiwa katika picha ya pamoja mapema leo mara baada ya kushiriki mkutano wa kujadili  maendeleo ya matumizi ya nishati karne ya 21 kwa nchi za Afrika,Mkutano huo uliowakutanisha Marais Wastaafu nane wa Afrika,umefikia tamati jana ndani ya chuo kikuu cha Witwatersrand, jijini Johannesburg, Afrika Kusini .Picha na Ahmed Michuzi-Johanneburg

Wabunge Wa Chadema Peter Msigwa na Joshua Nassari Nao Watua Washington DC


 Safari na muziki wameruka na wametua kwa salama na amani, wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kwanza kulia, Nassari Joshua, Dogo Janja akiwa na  Mhe.   Peter Msigwa ndani ya Washington DC
Wanachama wa Chadema Washington DC Anko Ludigo akiwa na Mhe Dogo Janja, Mkereketwa Libe aka Mwangombe, pamoja na Mhe. Peter Msigwa, wakiwa wameshikilia kadi za Chadema ambazo zipo tayari kwa kila  mwenye kupenda mabadiliko ya Tanzania.Picha na Picha na Libe Mwangombe
--
Ndani ya jiji la Washington Dc Wabunge  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)   waibuka jijini hapa kwa vishindo, huku Watanzania mbali mbali waishio nchini Marekani wakiwasuburi kwahamu siku hiyo ya Jumapili Mei 27, 2012,

Madhumuni ya mkutano huo ni kukutana na Watanzania wanaoishi Nchini Marekani kuzungumza juu ya mpango mzima  wa maendeleo  ya nchi yetu kwa jumla, mkutano huo utahudhuriwa na Mhe. Leticia  Nyerere, Mhe. Zitto Kabwe, Mhe. Nassari Joshua Marufu Dogo Janja na Mhe. Mchungaji Msigw